Maonyesho ya kilimo, mifugo na uvuvi yameanza rasmi katika viwanja vya nanenane Mkoani morogoro. Maonyesho haya yamekuja na kauli mbiu inayosema “Agenda 10/30 kilimo ni biashara, Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi”.

Pia katika maonyesho haya Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu imeshiriki kuwapatia wakulima na wafugaji elimu ya udhibiti wa viumbe hai waharibifu  mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ikiwemo udhibiti wa panya mashambani  kama vile mashamba ya mpunga, maharage na mashamba ya mahindi, udhibiti wa panya majumbani na ufugaji au utunzaji wa ndege aina ya Bundi  mashambani katika kupunguza baa la panya waharibifu.

Pamoja na haya Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu inatoa elimu kuhusu panya wanaotumika kubaini vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu na panya wenye uwezo wa kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini kwa kunusa.