Malaria ni miongoni mwa magonjwa tishio zaidi katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania hususani kwa watoto chini ya miaka mitano na kwa mama wajawazito. Tafiti kuhusu ugonjwa wa Malaria zaanza rasmi katika Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu.

 

Akitoa utambulisho wa mradi Dr. Amina Ramadhani Issae kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu amesema utafiti huu unaweza kusaidia kupunguza na kuondokana na ugonjwa wa malaria ikiwa ni mwendelezo wa tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto za magonjwa mbalimbali katika jamii. Utafiti huu utafanyika katika Mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilosa hususani katika vijiji vyenye changamoto kubwa ya Malaria.

 

Vijiji ambavyo vitanufaika na Mradi  huu wa malaria na vyandarua ni Unone, Makwambe, Zombo na Ihombe. Utafiti huu unalenga katika kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya vyandarua na mbinu mbalimbali za kupunguza mazalia ya mbu.