Watafiti kutoka Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu SUA (Institute of Pest Management (IPM)) walifanya ziara ya utafiti katika Mkoa wa Mjini Magharibi Wilaya ya Magharibi A Zanzibar wakishirikiana pamoja na watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo Zanzibar (Zanzibar Research Institute (ZARI)) kuanzia tarehe 21-25/03/2022
Madhumuni ya ziara hiyo ilikuwa ni kutoa mafunzo kwa maafisa ugani kutoka maeneo mbali mbali katika Mkoa wa Mjini Magharibi ili kuwajengea uwezo wa kuweza kutambua aina mbalimbali za wanyama waharibiifu na wasio waharibifu hususani panya, faida za kundi hili,hasara,na njia mbalimbali za udhibiti kwa wale panya waharibifu.Ziara hiyo ililenga vilevile kufunguwa ushirikianao kati ya taasisi hizi mbili (IPM na ZARI).
Akitoa utangulizi wa mafunzo hayo Kiongozi wa Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya (Africa Centre of Excellence for Innovative Rodent Pest Management and Biosensor Technology Development) kilichopo katika Taasisi ya Udhibiti Viumbe Hai Wahaaribifu –SUA, Prof. Apia Massawe alisema kwa muda mrefu kumekuwa na mashirikiano duni (gap) katika kujifunza na kutambuwa kundi hili kubwa la wanyama wadogo aina ya Panya kati ya taasisi zetu zilizoko Tanzania bara na Tanzania visiwani. Mafunzo haya yawe ni mwanzo wa kuunganisha nguvu zetu za kushirikiana katika tafiti hizi na kutafuta majibu ambayo yateleta tija kwa wakulima/wananchi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alieleza kuwa maafisa ugani ndio mkono mkubwa wa kufikisha tafiti zote kwa wakulima hivyo Taasisi na Serikali zinawategemea sana.
Mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa na Prof. Loth Mulungu wakishirikiana na Dr. Christopher Sabuni yalilenga mambo makuu yafuatayo:
- Njia mbali mbali zinazotumika kutambua aina za panya
- Faida mbalimbali za panya (mfano chakula, uwezo wa kunusa (biosensor technology)
- Hasara mbalimbali ziletazwo na panya (mfano uharibifu wa mazao, uhifadhi na usambazaji maradhi)
- Kutambua baadhi ya wadudu wanaoishi kwenye miili ya panya wanaoweza kueneza maradhi (kama viriboto, chawa, kupe) kutoka kwa panya kwenda kwa binadamu au mifugo
- Njia mbali mbali za kuweza kuthibiti panya waaharibifu kwa kutumia:
- Mitego
- Njia salama za kutumia viwatilifu (sumu sahihi) rodenticides
- Kutumia viumbe walao panya (biological control) kama bundi, nyoka, paka nk.
- Elimu ya kutunza na na kusafisha mazingira.
Mafunzo hayo yalikamilishwa na mafunzo ya vitendo ambapo maafisa ugani walioshiriki walifundishwa njia za kutega panya kuwakamata na kuwatambua aiana, jinsia, nk.
Mafunzo yalifungwa na Mkurugenzi wa ZARI Dr Mohamed Dhamir