BO Togel Bandar Togel Casino Online Bandar Togel Bandar Togel Toto Togel Daftar Togel Bandar Togel Terbesar Slot Gacor BO Togel
Mafunzo Ya Udhibiti Wa Panya Katika Mashamba Ya Mpunga – Afrirodents

Watafiti wa Taasisi ya  udhibiti viumbe hai waharibufu(SUA) Prof.Rhodes Makundi  akiambatana na watafiti wengine kutoka taasisi ya kudhibiti viumbe hai waharibifu, Madagasca na uingereza  watoa mafunzo ya udhibiti wa panya katika mashamba ya mpunga Ichonde na Kanolo  vilivyopo Wilayani Kilombero mkoani Mororgoro.

                             

Mafunzo haya yamehudhuliwa na wakulima na viongozi mbalimbali wa ngazi ya kata na kijiji cha Ichonde na Kanolo ambao ni wakulima wa mpunga katika bonde la mto Ichonde.Mafunzo haya yamekuja baada ya watafiti kubaini njia mbadala ambayo itawasaidia wakulima katika mapambano ya panya waharibifu wa mazao mbalimbali shambani kwa gharama nafuu kwa usalama wa afya ya wakulima na walaji.

Wakulima wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kukabiliana na panya wa mashambani ambazo zimekuwa zikighalimu kiasi kikubwa cha fedha na pia sio salama kwa afya zao na mifugo mbalimbali inayozunguka maeneo yao.

                               

“Wakulima wengi wamekuwa na changamoto ya mazao yao kuharibiwa na panya na wakulima wengine kutumia njia mbalimbali kudhibiti panya bila mafanikio.Kwa kutumia njia hii ya TBS(Trap barrier system) tunaweza kuondokana na tatizo ya mazao kuharibiwa na panya shambani na kuweza kupata mazao mengi na kukuza uchumi wetu pia” amesema Prof Makundi

Wakulima alipata fursa ya kuuliza maswali watafiti na kupatiwa majibu ya kuridhisha kuhusu namna bora ya kupambana na wadudu waharibifu mashambani.