Panya ni wanyama waharibifu wa mazao mengi yakiwemo mahindi na mpunga kuanzia shambani hadi ghalani. Hasara/upoteaji wa mazao shambani kutokana na athari za panya hutofautiana kutokana na maeneo na majira ya mwaka kwa sababu uwing wao pia hutofautiana kwa sehemu na majira ya mwaka pia. Kwa muda mrefu sasa, wakulima wamekua wakitumia viwatilifu (dawa zenye kemikali) ili kudhibiti panya. Lakini matumizi ya viwatifu hivyo yamekua na athari hasi nyingi kwenye afya ya viumbe hai na mazingira kwa ujumla.

Hivyo basi wazo la kutafuta njia ya kupunguza utegemezi wa viwatilifu visivyo salama kwa wanyama, binadamu na mazingira ili kudhibiti panya lilitakiwa. Wazo hili lilianza kufanyiwa kazi mnamo mwaka 2012 chini ya mradi maarufu kama “MRADI WA KUTUMIA HARUFU YA MKOJO WA PAKA” chini ya ufadhili wa kamishina ya sayansi na teknolojia (COSTECH). Malengo mkubwa wa mradi huu ni kutumia mkojo wa paka (Harufu yake) ili kuweza kufukuza panya katika mashamba na maghala ya kuhifadhia mazao ili kupunguza uharibifu wake.

Hadi sasa shughuli zilizofanyika ni kuweza kupata mkojo wa paka, kuupeleka maabara kwa uchunguzi zaidi na kuutumia katika mazingira ya wakulima kuona ufanyaji kazi wake. Matokea ya tafiti za maabara ni kwamba yarufu ya mkojo wa paka unafukuza panya katika eneo husika na hii inaonesha uwezo wa mkojo wa paka katika kuweza kufukuza panya. Lakini changamoto zilizopatikana ni upatikanaji mgumu wa mkojo wa paka na kuweza kupoteza nguvu/muda wa ufanyaji kazi kwa haraka Zaidi.

Hivyo basi, katika awamu hii, tafiti imelenga kutengeneza bidhaa yenye asili ya harufu ya mkojo wa paka itakayokuwa imeboreshwa na kutengnezwa kiwandani katika namna ya ufanisi wake na kurahisisha upatikanaji wake sokoni kwa ajili ya matumizi kirahisi.

Mkutano ulifunguliwa kwa utambulisho wa wajumbe waliohuhuria mkutano huu kutoka taasisi mbalimbali na wizara ya kilimo kama ifuatavyo;

  • Wilhelm Mafuru (Mkurugenzi mkuu) kutoka Wizara ya Kilimo na mafunzo
  • Loth S. Mulungu (Kiongozi wa mradi) kutoka Taasisi Ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA
  • C.A. Mgina kutoka Idara ya Kemia, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
  • M. Kichuki kutoka Ndaki ya Tiba ya Mifugo, SUA,
  • Prof A.S. Mwakalobo kutoka Idara ya Uchumi na Biashara, UDOM
  • Prof Apia W. Massawe kutoka Taasisi ya kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA
  • Elbert A. Mbukwa kutoka DUCE
  • Ashraf Mahmoud kutoka Farmers Centre LTD
  • Mashaka E. Mdangi (Makamu Mkurugenzi) Kutoka Wizara ya Kilimo na Mafunzo
  • Janeth Murro kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA
  • Miss Rehema Erasto kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA

Dr. Albert Mbukwa (DUCE) alifungua rasmi mkutano huu kwa kuishukuru Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu kwa kumpa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huu wa kitafiti. Amewasifu watafiti kutoka SUA kwa kuja na uvumbuzi wa teknolojia hii na kuweza kutengeneza bidhaa ambayo itapunguza matumizi ya viwatilifu kama vile sumu ya panya.

Utangulizi wa mkutano ulitolewa na Prof Loth Mulungu mtafiti kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu ambaye ni kiongozi wa mradi huu wa matumizi ya harufu ya mkojo wa paka katika kupambana na panya waharibifu mashambani na majumbani kwa usalama wa afya ya binadamu na viumbe wengine wanaoishi maeneo hayo.

Prof Mulungu amesema kwa sasa wakulima wengi wanatumia sumu katika kudhibiti panya ambazo siyo salama kwenye mazingira, binadamu na hazipatikani kwa urahisi pale zinapohitajika. Hivyo basi aliona ipo haja ya kuja na njia nyingine ya kudhibiti panya mashambani na manyumbani kama vile mkojo wa paka ambayo ni njia salama.

Katika kuona ubora wa wa teknolojia hii kama inafanyakazi kama ilivyokusudiwa, tafiti zilifanyika maabara, majumbani na mashambani na tafiti hizo zilitoa majibu mazuri ambapo ilionyesha kuwa panya wanaogopa harufu ya mkojo huo wa paka. kuweza kupima ubora .

Kwa upande wa Wadau wa Viwanda Bw. Ashraf Mahmoud kutoka Farmer Centre amesema wako tayari kufanya kazi na watafiti hawa kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu na kuwahakikishia kutoa huduma iliyo bora ili kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya watafiti na wadau wa viwanda.

Mkutano ulifungwa na Dr. Mafuru ambaye ni Mkurugenzi mkuu kutoka wizara ya kilimo na kusema kuwa wizara ipo bega kwa bega kuunga mkono juhudi za watafiti katika suala la kupambana na viumbe hai waharibifu mashambani ili kuweza kuwasaidia  wakulima kuondokana na matatizo ya wadudu waharibifu.

logo9_24_125214

The African Rodent Virtual Centre

Popular Link

Afrirodents© 2024. All rights reserved.