BO Togel Bandar Togel Casino Online Bandar Togel Bandar Togel Toto Togel Daftar Togel Bandar Togel Terbesar Slot Gacor BO Togel
Mkutano wa Kaimu Mkurugenzi Wakurugenzi na Watafiti Wastaafu wa Taasisi Ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu – Afrirodents

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu Prof. Mulungu amefanya mkutano na wakurugenzi  na watafiti wastaafu  wa Taasisi hii ikiwa ni baada ya aliyekuwa mkurugenzi wa taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibu Prof L.L Mnyone kuteuliwa wizarani.

Mkutano huu umehudhuriwa na wakurugenzi na watafiti wote waliomaliza muda wao wa uongozi na kujadili masuala mbalimbali ya kitafiti, kitaaluma na maendeleo ya taasisi kwa ujumla.

Aidha katika mkutano huu yamejadiliwa masuala mbalimbali ikiwemo  uundaji wa idara mbalimbali, ujenzi wa majengo ya taasisi, pamoja na kuongeza idadi ya wanataaluma na wafanyakazi wawezeshaji.

Kaimu Mkurugenzi amewashukuru sana wakurugenzi  na watafiti wastaafu kuhudhuria mkutano huu Pia wakurugenzi wastaafu wameahidi kushirikiana kwa karibu na Kaimu Mkurugenzi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.