Watafiti kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA wamefanya ziara ya kiutafiti katika Mikoa ya Pwani na kanda kusini ikiwa ni mwendelezo wa ziara za kitafiti ili kuangalia na kuidhinisha maeneo mapya ya Utafiti wa matatizo yanayosababishwa na panya.  Watafiti hao Prof. Apia Massawe na Prof. Loth Mulungu wamesema  ziara hii imelenga katika kutimiza yafuatayo:

  1. Kutafuta maeneo ambayo yanafaa kufanyia tafiti mbalimbali zinazohusu ikolojia  ya panya kwenye mikoa ya pwani ya bahari ya hindi
  2. Kuidhinisha maeneo ya tafiti kuhusiana na panya wanaopatikana kwenye mikoa inayozunguka bahari ya hindi
  3. Kuangalia mazingira asili kama misitu, vichaka, maeneo ya miinuko na ya tambarare ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti ili kugundua aina mpya za panya
  4. Kujionea maeneo yanayotumika kwa shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji ambapo kunatokea milipuko ya panya ili kugundua aina ya panya waliopo na kinachosababisha milipuko hiyo
  5. Kufanya utafiti juu ya magonjwa yanayobebwa na kusababishwa na panya kwa binadamu, n.k.

Watafiti wa SUA  wametembelea Mkoa wa pwani ,Lindi, Mtwara, Songea na Njombe na kusema kuwa tafiti zote hizi zitafanywa na wanafunzi wa Shahada ya Kwanza na ya pili wanaofadhiliwa  na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya (ACE IRPM &BTD).

Aidha Prof. Apia Massawe amesema kuwa kutoka na mwonekano wa ikologia ya sehemu mbalimbali za Mkoa wa mtwara, ikichangiwa pia na hali ya hewa  inawezekana panya waliopo wakawa  wamebeba vimelea vya magonjwa kama tauni.

Inajulikana kuwa bakteria wanaosabisha ugonjwa wa Tauni wanaweza kuwepo wanazunguka ndani ya miili ya panya kwa muda wa miaka mingi bila milipuko  kutokea kwa binadamu. Aidha, kama kutatokea mabadiliko yanayosababishwa na shughuli za binadamu au mabadiliko yanayotokana  na tabia nchi ugonjwa unaweza kujitokeza kwa upya ndani ya jamii na kuleta milipuko kwa upya

logo9_24_125214

The African Rodent Virtual Centre

Popular Link

Afrirodents© 2024. All rights reserved.